ACT WAZALENDO,CHADEMA WAIKATAA RIPOTI YA JAJI CHANDE

Na Ally Mandai. 

 Chama cha ACT Wazalendo kimefuatilia uwasilishwaji wa Taarifa ya Tume ya Uchunguzi wa Mauaji ya Oktoba 2025 iliyowasilishwa leo. Chama kinasimama imara katika msimamo wake wa kukataa kile kinachoitwa Tume ya Chande, ambayo tangu mwanzo tulieleza kuwa haina uhuru na imeundwa kama chombo cha kulinda wahusika badala ya kutoa haki. Msimamo wetu huo umethibitika leo.

Ripoti iliyowasilishwa leo na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Ndg. Mohamed. Chande Othman kwa Rais Sania Suluhu Hassan ina hitimisho ambalo lilitarajiwa kabisa kutokana na muundo wake, wajumbe wake na hadidu rejes za Tume hiyo.

ACT Wazalendo tunaombeleza kila maisha yaliyopolezwa na kila familia iliyopata madhila kufuatia matukio ya tarehe 29 Oktoba na athari zake. Uponyaji wa kweli wa taifa na maridhiano ya dhati yanaweza kupatikana tu kupitia uchunguzi huru, wa kuaminika na ulio wazi.

Tumeshangazwa kusikia kuwa baada ya Tume ya Jaji Chande, sasa kutaundwa Tume nyingine. kufanya uchunguzi wa kijinai wa matukio yale yale. Hii ni ujanja ujanja mwingine wa kupoteza muda mwingine na kutafuna fedha za walipa kodi. Watanzania hawawezi kukubali ulaghai na ujanja ujanja wa aina hii

ACT Wazalendo tunarudia wito wetu wa kuundwa kwa uchunguzi huru wa kimataifa chini ya taasisi zenye kuaminika kama Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika au SADC

Hii ni kauli yetu ya awali. Msimamo wa kina zaidi utakaoangazia maeneo yote utatolewa baada ya kikao cha Kamati ya Uongozi ya Chama Taifa itakayoketi hivi karibuni katika kipindi cha wiki moja.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinarejea msimamo wake wa awali wa tarehe 19 Novemba 2025 kutotambua mchakato mzima wa Tume iliyoundwa na Samia Suluhu Hassan, na kinapinga kwa ujumla wake ripoti iliyowasilishwa leo tarehe 23 April 2026 na Tume hiyo chini ya Jaji Mohamed Chande Othman.

CHADEMA inasisitiza kuwa, kwa mujibu wa kauli ya wazi ya Samia Suluhu Hassan mwenyewe, ripoti hiyo ni yake binafsi. Hivyo, haiwezi kuchukuliwa kama nyaraka huru yenye kuakisi ukweli au haki kwa waathirika wa matukio yaliyoripotiwa.




Post a Comment

0 Comments