YOWERI MUSEVENI ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA EAC

 Na Ally Mandai.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akipokea kijiti cha uongozi kutoka kwa mtangulizi wake Rais wa Kenya, William Ruto.

Nafasi hiyo ya Uenyekiti wa Museveni, imetangazwa leo Machi 7, 2026 Jijini Arusha katika Mkutano wa Kawaida wa 25 wa wakuu wa nchi wa jumuiya hiyo unaoendelea jijini humo.

Museveni anachukua nafasi hiyo, huku akitarajiwa kuongoza ajenda za kuimarisha ushirikiano wa kikanda, kukuza uchumi na maendeleo ya pamoja ya nchi wanachama wa EAC.


 

Post a Comment

0 Comments