Na Ally Mandai.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan leo ametoa salamu za heri na pongezi kwa wanawake wote nchini ikiwa ni sehemu ya kusheherekea siku ya kimataifa ya wanawake.
"Ninawapongeza
na kuwatakia kheri wanawake wote katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa
ya Wanawake. Siku hii inatupa fursa ya kipekee ya kutambua, kujivunia na
kusherehekea mafanikio tuliyopata, hasa katika elimu, afya, uchumi na
uongozi".
"Siku hii inatukumbusha pia wajibu wetu wa msingi kwa
waasisi wetu na kwa vizazi vya sasa na vijavyo; wa kuendelea kupanga na
kutekeleza mipango ya kumwezesha mwanamke, ikiwa ni sehemu muhimu ya
kazi ya kukomboa familia, jamii na Taifa kwa ujumla".

0 Comments