YANGA YATAKATA SINGIDA,AZAM YABANWA SOKOINE

 Na Ally Mandai.

Yanga SC wametakata kwenye uwanja wa Airtel Singida kufuatia ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Singida Black Stars,Huku Azam FC ikishindwa kutamba dhidi ya Tanzania Prisons katika dimba la Sokoine, Mbeya kufuatia sare tasa.

Yanga SC wameendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa NBC sasa wamefikisha jumla ya alama 32.

Azam FC wamesogea mpaka nafasi ya 4 kwenye msimamo wakimshusha Pamba Jiji na wamefikisha jumla ya alama 24 huku wote wakiwa sawa kwa alama utofauti ni magoli ya kufunga na kufungwa.

FT: Singida Black Stars 0-3 Yanga Sc

 39' Dube

 45+2' Okello

 54' Mudathir

FT: TZ Prisons 0-0 Azam FC.


TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804.



Post a Comment

0 Comments