MTOTO WA NABII MWAMPOSA AJIUNGA NA YANGA SOCCER SCHOOL

 Na Ally Mandai.

Kwenye usaili wa Vijana watakaojiunga na Yanga Soccer School Leo kwenye Viwanja vya Gymkhana, Mtoto wa Mchungaji Mwamposa, Prince Hamis Mwamposa amekuwa miongoni mwa vijana waliowasili kwenye eneo hilo kwaajili ya kufanya usaili wa kujiunga na Yanga Soccer School

Prince Hamis Mwamposa amesema kuwa yeye ni Shabiki wa Yanga na ilikuwa ndoto yake kujiunga na klabu hiyo.

Pia amefunguka kuwa yeye aanavutiwa na jinsi anavyo cheza nyota wa Ivory Coast na klabu hiyo,Pacome Zouzoua.

"Kwa Pacome napenda anavyo dribble mpira,anatulia akiwa mchezoni na wala hapendi ugomvi ndio ninavyopenda" alisema.

TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804. 



Post a Comment

0 Comments