MAGANYA AAGIZA HUDUMA BORA ZITOLEWE KWA WANANCHI

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Fadhili Maganya, ametoa onyo  kwa watumishi wa umma Wilaya ya Mbinga  Mkoani Ruvuma akisisitiza utoaji wa huduma bora, kwa wakati na kwa lugha yenye staha akisema ubora wa huduma ndiyo kipimo cha imani ya wananchi kwa Serikali.

Akizungumza katika kikao cha viongozi wa chama na Serikali kilichofanyika Mbinga DC Mall, Maganya alibainisha kuwa kasi ya maendeleo lazima iendane na heshima kwa mwananchi. Alifikisha pia salamu za Rais, akiahidi kuendelezwa kwa uwekezaji wa miradi ya maendeleo.

Ameelekeza hospitali zote kuweka dirisha maalum la huduma kwa wazee kulingana na ilani ya chama. Aidha, amesisitiza uwiano wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, akitaka kila kata kunufaika bila upendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa , Kisare Makori, amesema Mbinga ina hali ya amani na ukuaji wa uwekezaji, ikiwemo ujenzi wa hoteli tatu, na kutoa mwaliko kwa wawekezaji wapya.



Post a Comment

0 Comments