ATHARI YA BOMU LA NYUKLIA

Kila ifikapo tarehe 6 Agosti, dunia inakumbuka  athari kubwa ya bomu la nyuklia iliotokea mwaka 1945, katika vita kuu ya pili ya dunia. Watu walishangazwa na athari zilizotokea katika mji wa Hiroshima, Japan. 

Zipo sababu nyingi ambazo zilipelekea kutokea kwa bomu la nyuklia, ikiwemo mwaka 1941, baada ya Japani kushambulia kituo cha jeshi cha marekani huko Hawaii,  na kusababisha wanajeshi na meli nyingi za Marekani ziliharibiwa. 

Marekani ilichagua kushambulia Hiroshima  kwasababu ilikuwa kituo kikuu cha jeshi la Japan na walikuwepo watu wengi wanaendesha shughuli za kawaida.   Bomu la Nyuklia aina ya "Little Boy" lilipandishwa na ndege aina ya Enola Gay kutoka Tinian, Pacific. Na kufikia majira ya saa 8:15 asubuhi lililipuka katika mji wa Hiroshima na kupelekea athari kubwa, watu zaidi ya 70,000+ walipoteza maisha hapo hapo na maelfu ya watu walifariki baadaye kutokana na  mionzi ya nyuklia. 

Baada ya kutokea kwa bomu hilo watoto wengi walizaliwa wakiwa na tatizo la afya( vilema), lakin pia yalitokea madhara makubwa ya magonjwa kama saratani hivyo mpaka sasa nchi nyingi zilijifunza kitu kutokana na athari hizo. 

Baada ya mashambulio makubwa yalioendelea kufanyika, tarehe 15 Augost 1945, mfalme wa Japan ( Hirohito ) alitangaza kupitia redio kuwa Japan inajisalimisha.  Hata ilipofikia September 2, 1945 Japan ilisaini rasmi hati ya kujisilimisha na kupelekea kuisha kwa vita  kuu ya pili ya dunia kuisha.

Je, kutokana na madhara yaliotokana na nyuklia  kwasasa marekani iko sahihi kumpinga Iran   kuhusu uzalishaji wa mabomu ya Nyuklia?



Post a Comment

0 Comments