AS FAR RABAT YASITISHA SAFARI YA PYRAMIDS LIGI YA MABINGWA AFRIKA

 Na Ally Mandai.

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Pyramids ya Misri, wameaga rasmi mashindano hayo baada ya kufungwa kwa jumla ya mabao 3-2 na AS FAR Rabat ya Morocco katika hatua ya robo fainali.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza, timu hizo zilimaliza kwa sare ya 1-1, lakini AS FAR Rabat walionyesha ubora wao kwenye mechi ya marudiano kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kufuzu kwa hatua ya nusu fainali.

Kwa ushindi huo, AS FAR Rabat sasa wanasonga mbele kusubiri mshindi kati ya RS Berkane na Al Hilal Omdurman, watakaokutana kesho kuwania tiketi ya hatua hiyo.

Matokeo ya mechi:

FT: Pyramids 🇪🇬 1-2 🇲🇦 AS FAR Rabat (Agg. 2-3)

⚽ 09' Reda Slim

⚽ 54' Hrimat

⚽ 63' Mayele



Post a Comment

0 Comments