https://otieu.com/4/10556571 ZOEZI LA KUDHIBITI MAMBA HATARI LAENDELEA MTO RUVU, KIBAHA DC

ZOEZI LA KUDHIBITI MAMBA HATARI LAENDELEA MTO RUVU, KIBAHA DC

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imefanikiwa kudhibiti mamba hatari katika Mto Ruvu, Kijiji cha Ruvu Stesheni, leo tarehe 02 Januari 2026.

Wakizungumza wakati wa tukio hilo, Maafisa Wanyamapori wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Lameck Makuwe na Peter Kisaka, wamesema kuwa zoezi la uvunaji wa mamba sumbufu bado linaendelea usiku na mchana. Hivyo, wametoa wito kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa Mto Ruvu kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya wanyama hatari.

Maafisa hao wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujilinda dhidi ya wanyama wakali, ikiwa ni pamoja na kulinda usalama wao na mifugo yao.

Kwa upande wao, wananchi wamemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Bi. Regina L. Bieda, kwa kuhakikisha wataalamu wanawafikia kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi hivyo Wananchi  wameeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa halmashauri.

Aidha, namba za mawasiliano za Maafisa Wanyamapori zimetolewa kwa wananchi ili kurahisisha utoaji wa taarifa pale hali hatarishi inapojitokeza.

Maafisa Wanyamapori wamewahimiza wananchi kutoa taarifa mara moja wanapokumbana na wanyama hatarishi, ili hatua za haraka zichukuliwe.






 

Post a Comment

0 Comments