SIMBA OUT LIGI YA MABINGWA,TUKUTANE MWAKANI

Na Ally Mandai.

Ndoto ya Simba SC kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika imefikia tamati rasmi baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Petro de Luanda ya Angola.

Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha jumla ya alama 2 pekee katika msimamo wa Kundi D, hali iliyowafuta moja kwa moja kwenye mbio za kusonga mbele huku wakibaki mkiani mwa kundi hilo.

Licha ya kupambana kwa dakika zote 90, wekundu wa Msimbazi walishindwa kupata ushindi waliouhitaji ili kufufua matumaini yao, na sasa safari yao katika mashindano hayo imefikia mwisho mapema.

Kutolewa kwa Simba kunazidi kuipa uzito kauli mbiu ya mashabiki juu ya mwenendo wa timu katika michuano ya kimataifa, huku macho sasa yakielekezwa kwenye marekebisho ya kikosi na maandalizi ya mashindano yajayo.

Wanamsimbazi, maoni yako yakoje? Tatizo ni benchi la ufundi, wachezaji au maandalizi kwa ujumla au Uongozi ? 





Post a Comment

0 Comments