Na Ally Mandai.
Timu ya Simba SC imeendelea kukumbana na matokeo yasiyoridhisha katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Esperance ya Tunisia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Matokeo hayo yameifanya kauli mbiu ya “Kwa Mkapa Hatoki Mtu” kuonekana kupoteza makali, kwani Simba bado haijapata ushindi wowote katika hatua ya makundi msimu wa 2025/26.
Katika mchezo huo, Simba ilitangulia kupata mabao mawili ya mapema, lakini ilishindwa kuyahifadhi, ikiruhusu Esperance kusawazisha kabla ya filimbi ya mwisho.
Kwa sasa, Simba inabaki mkiani mwa Kundi D ikiwa na pointi 3, huku Stade Malien ikiongoza kwa pointi 8, ikifuatiwa na Esperance yenye pointi 6 na Petro Atlético yenye pointi 5.



0 Comments