Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma @mwanafa ameungana na waombolezaji katika msiba wa nguli wa muziki wa dansi nchini, Mzee Stephen Hiza (80) leo Februari 18, 2026 jijini Tanga.
Mzee Hiza atakumbukwa daima kwa mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa Tanzania, hususan kupitia wimbo wake maarufu wa "Tanzania Yetu ndiyo Nchi ya Furaha," ambao umebeba hisia nzito za uzalendo na mshikamano wa kitaifa.



0 Comments