MAVUNDE AZINDUA KISIMA CHA MAJI MSALATO, AWATAKA WANANCHI KUKILINDA

 Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Msalato Ubalozi wa Catherine Mwajoka wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji kwa ajili ya matumizi ya wananchi ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi ambayo Mbunge Mavunde aliitoa kwa wananchi wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025 juu ya upatikanaji maji safi na salama.

Mbunge Mavunde amewataka wananchi wa mtaa wa Msalato kulinda na kuitunza miundombinu ya kisima hicho cha maji na kuahidi kuendelea kutatua changamoto mbalimbali.

Aidha,Mh. Mavunde aliwashukuru wananchi wa Msalato kwa imani kubwa na kura walizompigia Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan,Mbunge na Diwani wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025.







 

Post a Comment

0 Comments