KESI YA UHAINI YA LISSU YAHAIRISHWA HADI FEBRUARI 11

Na Ally Mandai.

Kesi ya uhaini Na. 19605/2025 dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu imeahirishwa hadi Jumatano, Februari 11, 2026, ambapo Mahakama itatoa uamuzi juu ya mapingamizi yaliyowasilishwa.

Leo Februari 9, 2026 upande wa Jamhuri uliwasilisha majibu ya mapingamizi yaliyowasilishwa na mshtakiwa Novemba 12, 2025, yanayohusu matumizi ya shahidi wa siri wa Jamhuri pamoja na uwepo wa kizimba maalum cha kutolea ushahidi wa siri ndani ya chumba cha mahakama.






Post a Comment

0 Comments