https://otieu.com/4/10556571 DC NGUBIAGAI AWAASA WANANCHI KUTUMIA NJIA HALALI KUTAFUTA HAKI

DC NGUBIAGAI AWAASA WANANCHI KUTUMIA NJIA HALALI KUTAFUTA HAKI

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cde.Christopher Ngubiagai amewaasa wananchi wa Ukerewe kutumia njia halali kutafuta haki na kuepuka njia za mkato zinazowakutanisha na wanasheria wasio sahihi.

Ameyasema hayo wakati wa kilele cha madhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika leo Februari 02,2026 katika viwanja vya Mahakama ya wilaya ya Ukerewe yakihudhuriwa na wadau mabalimbali wa sheria, asasi za kijamii na wananchi yakilenga kuimarisha haki kwa maendeleo ya jamii ya Ukerewe na taifa kwa ujumla.

"... ni vema mkatumia njia halali za kutafuta haki muepuke kujichukulia sheria mkononi mtumie vyombo halali badala ya visasi, fitina na maneno ya mitandaoni, mahakama si adui wa mwananchi bali ni adui wa kuvunja sheria..." Amesema.

Akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa mahakama ya Ukerewe Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Mhe. Ally Bushiri amesema mahakama imefanikiwa kulinda haki za binadamu kama zilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 13-29 na sheria za kimataifa, imedumisha utawala wa sheria, imetatua migogoro mbalimbali ya kodi na uwekezaji, imewaadhibu wenye makosa ya jinai, imelinda makundi maalum na kusimamia haki za kisiasa.

Nae mwakilishi wa Chama cha mawakili (TLS) wakili msomi Charles Mkaima amewasihi wananchi kutoamini mawakili vishoka wasio na sifa katika kuendesha kesi zao, wafike mahakamani kupata wataalam ili kupata haki itakayotokana na taaluma sahihi kutoka kwa wataalam wa sheria.

Kwa upande wake mwakilishi wa TAKUKURU wilaya ya Ukerewe Ndg. William Mapunda amewaasa wananchi kuzifahamu sheria za nchi, kuepuka kupokea na kutoa rushwa na kutoa taarifa za uhalifu ,kuwa tayari kutoa ushahidi mahakamani pale itakapobidi.

Elizabeth Adam ni mkazi wa kijiji cha Nkilizya yeye amepongeza juhudi za mahakama kuwashirikisha wananchi kupitia mafunzo mbalimbali huku akiahidi kuwa balozi kwa wananchi wengine kushiriki katika mafunzo ya kisheria yanayotolewa nyakati mbalimbali.






 

Post a Comment

0 Comments