Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda leo februari 10, 2026 amehutubia Baraza la Madiwani lililofanyika katika Ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo Manispaa ya Temeke.
Akizungumza katika Hotuba yake Mhe. Mapunda amewataka Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha kuwa kila jambo ambalo Mheshimiwa Diwani atalifanya kwenye Kata yake liendane na Matakwa ya Manispaa na liwe na Manufaa kwa Manispaa nzima ya Temeke.
" Utekelezaji wa kila jambo kwa Diwani lazima unufaishe Manispaa nzima ya Temeke, huu ndiyo wajibu wetu lazima tubadilike", alisema DC Mapunda.
Aidha, DC Mapunda amehimiza utekelezaji wa Maagizo yote yaliyotolewa na yanayoendelea kutolewa na Wakuu wa Nchi ili kuhakikisha Manispaa ya Temeke inaenda sambamba na Dira ya maendeleo ya Taifa.
Kadhalika, DC Mapunda amewahimiza Waheshimiwa Madiwani kuwa na mipango ya muda mrefu na yenye tija ili kuweza kuleta Maendeleo zaidi katika Manispaa ya Temeke.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
0 Comments