Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi kimesema kimepokea taarifa ya maendeleo ya mazungumzo yanayotafuta Muafaka wa utatuzi wa Kisiasa yenye lengo la kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.
Aidha, CCM kimetaja mazungumzo hayo kuwa bado siri huku yakisimamiwa na Marais Wastaafu wa Zanzibar , Dk Amani Abeid Karume na Dk Ali Mohamed Shein.
Hayo ameyaeleza Katibu Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar, Cde: Khamis Mbeto Khamis, Ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya uwepo wa mazungumzo baina ya ACT na Wazalendo baada ya kukamilika kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu Taifa kilicho fanyika tarehe 19/2/2026 katika Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar,
Mbeto alisema Msingi wa mazungumzo hayo , umejiegemeza katika kuzipitia hitilafu, dosari na kasoro mbambali za Kisiasa na Kisheria , hatimae ziweze kurekebishwa .
Alisema pia katika Majadiliano hayo zitaangaliwa kasoro na dosari endapo ni za kisheria , zitapelekwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kufanyiwa Marekebisho ya kisheria kwa mujibu wa katiba ya zanzibar ya mwaka 1984.
"Kamati Maalum ya NEC Zanzibar imepokea taarifa ya kuendelea kwa mazumgumzo kati ya CCM na ACT . Agenda za mjadala huo bado ni siri . Hatma ya mazumgumzo hayo ikifikiwa itatangazwa na pande zote mbili" Alisema Mbeto
"Katika Majadiliano ikiwa kutaonekana haja ya kubadili jambo husika kisheria , suala hilo litapelekwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kwa mfano huwezi kuondosha
Kura ya mapema bila kubadili sheria yake. "Alisema Mbeto
Katibu huyo Mwenezi alisema ni majadiliano yenye nia njema kwa mustakabali na ustawi wa Zanzibar na Wananchi wake .
"Wajumbe Washiriki kwenye mazungumzo hayo watarudisha mrejesho kwa chama kilichowatuma. Hatua nyingine za Vikao vya juu vya chama chetu zitafuata na kutoa maamuzi yake "Alisema Mbeto
.jpeg)
0 Comments