𝗪𝗔𝗦𝗜𝗖𝗛𝗔𝗡𝗔, 𝗣𝗘𝗡𝗗𝗘𝗡𝗜 𝗦𝗔𝗬𝗔𝗡𝗦𝗜 𝗜𝗡𝗔 𝗙𝗨𝗥𝗦𝗔 𝗡𝗬𝗜𝗡𝗚𝗜 - 𝗠𝗛𝗘. 𝗠𝗔𝗛𝗨𝗡𝗗𝗜

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amehimiza wasichana kupenda masomo ya sayansi na kushiriki kikamilifu katika taaluma hizo kutokana na manufaa yake kwa maisha yao na maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi yaliyofanyika jijini Dodoma Februari 11, 2026,  Mhe. Mahundi amesema sayansi inawawezesha wanawake na wasichana kujenga uwezo wa kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Mhe. Mahundi amebainisha kuwa,  Serikali inaendelea kutekeleza mikakati ya kuondoa vikwazo vinavyowazuia wanawake na wasichana kushiriki katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi ili kuleta usawa wa kijinsia.






 

Post a Comment

0 Comments