Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara amesema kuwa serikali inaendelea kuwekeza kwenye bandari ya dar esalaam ikiwa ni kutokana na ongezeko la Meli kubwa kuingia katika bandari hiyo hivyo imesababisha shehena ya Mzigo kuongezeka huku wadau wa Bandari wametakiwa kuchukua mizigo yao kwa wakati ili kutoa fursa kwa Mizigo mingine iweze kuhudumiwa kwa wakati.
Akizungumza Jijini Daresalaam kwenye kikao cha wadau wa Maboresho ya Bandari Katibu Mkuu wizara ya uchukuzi Profesa Godius kahyarara amewataka wadau wa Bandari na Taasisi mbalimbali za Serikali na Sekta binafsi kushirikiana katika kutoa huduma wakiwemo TRA, TASHICO,TTFCA, TBS , Wamiliki wa Maroli, Wizara ya mambo ya Ndani, TAMISEMI na Wizara ya Uchukuzi.
“Serikali inaendelea kuwekeza zaidi katika bandari ya Dar es salaam kwa kuboresha na kuongeza kina cha mlango wa bahari, ujenzi wa magati na ununuzi wa vifaa na kushirikisha sekta binafsi ambapo imepelekea kuongeza shehena katika bandari ya Da er Salaam”alisema Kahyarara.
Kwa upande wake Meneja wa Bandari ya Dar es salaam Abed Gallus ameongeza kuwa kutokana na kuongezeka kwa shehena hasa Makasha (Conteina) Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) wanaendelea na upanuzi wa maeneo mengine kwa ajili ya kuhifadhia Makasha hayo. Pia ICDs nyingi zimejaa hivyo mamlaka hiyo inaongeza maeneo kama vile EPZA ili kuweka Makasha.
Naye Meneja wa Undeshaji kutoka Shirika la reli Tanzania (TRC )Focus Sahani amesema kwa sasa Serikali imenunua vichwa nane kwa ajili ya kupeleka Makasha katika Bandari Kavu ya kwala ambapo vichwa viwili tayari vimeanza kazi na vichwa sita vipo katika majaribio.
.jpeg)

.jpeg)
0 Comments