Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ilimtembelea Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, nyumbani kwake Kawe Beach jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kumpa pole kufuatia msiba wa shemeji yake, ambaye ni dada wa mke wake, Mama Salma Kikwete, uliotokea hivi karibuni.
Akizumgumza na ujumbe huo wa TAWA Dkt Kikwete aliipongeza TAWA kwa kazi kubwa na nzuri wanaendelea kuifanya ya kulinda na kusimamia rasilimali za wanyama pori nchini pamoja na mchango wa TAWA katika kukuza sekta ya Utalii.
Aidha alielezea kuridhishwa kwake na juhudi za mamlaka hiyo za kuendeleza uhifadhi endelevu na wenye manufaa makubwa kwa taifa.
Katika mazungumzo na na Ugeni huo, Rais Mstaafu Kikwete alionesha nia na hamu ya kutembelea baadhi ya vivutio vya Utalii vinavyosimamiwa na TAWA.
Amevutaja vivutio hivyo kuwa ni pamoja na Magofu ta Kilwa yaliopo Kilwa Kisiwani ambayo yana mchango mkubwa katika Utalii na Historia ya Tanzania.
Mapema katika ziara hiyo, Rais Mstaafu Dkt. Kikwete aliwasilisha changamoto inayomkabili yeye na familia yake kuhusu uwepo wa wanyama aina ya Nguchiro, ambao wamekuwa wakisababisha usumbufu katika makazi yake.
Akielezea hali hiyo alisema:
“Mimi na mke wangu tumefurahia sana ujio wenu kwa sababu tuna imani mtatusaidia pia kutatua changamoto tunayopitia. Tumekuwa tukisumbuliwa sana na Nguchiro; awali hapa nyumbani tulikuwa tunafuga kuku na tulikuwa nao wengi sana, lakini kwa sasa wote wamemalizwa na nguchiro.
Kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Mlage Yusuf Kabange, ugeni huo ulimkaribisha rasmi Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kutembelea vivutio vyote vinavyosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini, huku ukimhakikishia kuwa mamlaka hiyo iko tayari kushirikiana na kuchukua hatua stahiki katika kushughulikia changamoto ya Nguchiro aliyoiwasilisha.
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
0 Comments