Na Ally Mandai.
Klabu ya Simba SC imeendelea kupoteza michezo ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi baada ya leo kufanya hivyo tena dhidi ya Espérance Sportive de Tunis nchini Tunisia kwa bao 1-0 likifungwa kipindi cha kwanza cha mchezo.
Simba SC kwa sasa inashikilia mkia kwenye msimamo wa kundi D ikiwa haina alama yoyote na kwenye magoli wana -3 huku vinara wakiwa Espérance de Tunis wenye alama 5,wakifuatiwa na Petro Luanda wenye alama 4 na Stade Malien wenye alama 4 pia.
Licha ya kufanya usajili mpya kikosini lakini bado hali ni tete na sasa wamebakisha michezo mitatu ya kurejesha matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali huku ligi kuu pia mambo yakiwa magumu sasa wanashika nafasi ya 5 kwenye msimamo.
We una shauri kipi kifanyike kurejesha makali ya mnyama Simba SC??



0 Comments