Baraza la Mawaziri chini ya uongozi wa Rais wa mpito Ibrahim Traoré lilipitisha amri (décret) ya kuvunja vyama vyote vya siasa na kuondoa sheria zilizokuwa zinazidhibiti shughuli zao.
Vyama vingi (zaidi ya 100 kabla ya mapinduzi) vimesababisha mgawanyiko na kudhoofisha umoja wa taifa.
Hatua hii ni sehemu ya "kujenga upya taifa" na kurekebisha mfumo wa siasa wakati nchi inakabiliwa na changamoto za usalama (magaidi).Mali yote ya vyama itachukuliwa na serikali.
Wafuasi wa Traoré wanasema ni hatua ya kimapinduzi kufuata mfano wa Thomas Sankara ili kuondoa ushawishi wa ubeberu na kuleta umoja. Wakosoaji wanasema inaimarisha udikteta wa kijeshi na kuua uhuru wa kisiasa.

0 Comments