MATWEBE AMPA KONGOLE MAKONDA KATIKA KUWAKUMBUKA WANAMITANDAO WALIOJIAJIRI.

Na Moshi saidi

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), Shaban Omary Matwebe, amempongeza Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, kwa hatua yake ya kuahidi kupigania upatikanaji wa mikopo kwa vijana waliojiajiri katika sekta ya habari za mitandaoni.


Matwebe amesema mpango huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwawezesha vijana wanaomiliki na kuendesha Online TV pamoja na majukwaa mengine ya habari za kidijitali kununua vifaa vya kisasa, hivyo kuongeza ubora wa maudhui yao na ushindani katika soko la habari.

Aidha, amemuomba Waziri Makonda kuendelea kupambana ili kuhakikisha mitandao ya kijamii kama Instagram na TikTok inaanza kuwalipa watumiaji wake nchini Tanzania, kama ilivyo katika baadhi ya nchi nyingine duniani, hatua ambayo itatoa fursa zaidi za kipato kwa vijana wabunifu na watayarishaji wa maudhui.

Kwa mujibu wa Matwebe, utekelezaji wa ahadi hizo utachochea ukuaji wa sekta ya habari za mitandaoni, kuongeza ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa kidijitali nchini.


Post a Comment

0 Comments