Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Gugu, amewataka wafanyakazi wa Wizara hiyo kuendelea kudumisha mshikamano, upendo na ushirikiano kazini, akisisitiza kuwa umoja wao ndio msingi wa ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali.
Gugu ameyabainisha hayo wakati akifungua rasmi Kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha Wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msalato, jijini Dodoma, leo Januari 10, 2026.
Akizungumza katika kikao hicho, Gugu amesema kuwa Baraza la Wafanyakazi ni jukwaa muhimu linalowawezesha watumishi kushiriki kikamilifu katika masula muhimu ya utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Ameeleza kuwa kikao hicho ni cha kwanza kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na kimeandaliwa mahsusi kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa mpango wa bajeti wa Wizara katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Disemba, 2025 pamoja na kujadili mikakati ya utekelezaji kwa kipindi kinachofuata.
Kadhalika, Gugu amesisitiza umuhimu wa viongozi na wafanyakazi kuendelea kushirikiana na kusaidiana katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, akieleza kuwa kudumisha utu, maadili mema na utendaji kazi wenye staha utaisaidia Wizara ya hiyo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na tija zaidi.


.jpeg)

0 Comments