Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. 𝗔𝘀𝗵𝗮-𝗿𝗼𝘀𝗲 𝗠𝗶𝗴𝗶𝗿𝗼 amewataka Mabalozi wa mashina kutokuwa watu wa kupokea tu amri kutoka juu na badala yake amri zitoke chini kuja juu kwakuwa wao ndiyo wenye kuwajua wanachama maana ndipo chimbuko la wanachama linapoanzia.
Dkt. Migiro ameyasema hayo tarehe 7 Januari 2026 wakati wa kuanza kwa ziara yake ya kukutana na Mabalozi wa mashina ambapo ameanza na wilaya za Temeke na Kigamboni Jijini Dar es salaam.
Akizungumza mbele ya maelfu ya Mabalozi hao, Dkt. Migiro ametanguliza shukrani kwa Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu. Kenani Kihongosi kwa kuwa mlezi bora wa kichama wa mkoa wa Dar es salaam na kwa kufanya ziara yake aliyotoa nasaha na kuhamasisha namna ambavyo ngazi itoke chini kwenda juu na sio juu kushuka chini.
Akiweka mkazo juu ya umadhubuti na uimara wa CCM, Dkt. Migiro amesema kuwa ngazi ya mashina na kata ndipo umadhubuti na uimara wa Chama Cha Mapinduzi unapoanzia hivyo ni muhimu zaidi Mabalozi wa mashina kuzingatia hilo na pia kushauri ni namna gani iliyobora ya kushirikiana ili kutimiza adhma ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 ya kuhakikisha CCM inakuwa imara siku hadi siku.
Aidha, Balozi Dkt. Migiro amesema Mabalozi na Viongozi wote wana wajibu wa kurejea mambo mazuri yaliyofanywa katika kutekeleza ilani ya CCM kwa miaka 5 iliyopita na hata kwa kipindi hiki cha miezi miwili tangu kuisha kwa uchaguzi mkuu.
Vilevile, Dkt. Migiro ameweka wazi kuwa umati wa Mabalozi waliojitokeza unaendelea kutuma salamu kuwa itikadi ya CCM inaendelea kukua siku hadi siku.
"𝘜𝘮𝘢𝘵𝘪 𝘩𝘶𝘶 𝘸𝘢 𝘸𝘢𝘵𝘶 𝘸𝘢 𝘳𝘪𝘬𝘢 𝘮𝘣𝘢𝘭𝘪𝘮𝘣𝘢𝘭𝘪 𝘩𝘶𝘬𝘶 𝘷𝘪𝘫𝘢𝘯𝘢 𝘸𝘢𝘬𝘪𝘸𝘢 𝘸𝘦𝘯𝘨𝘪 𝘻𝘢𝘪𝘥𝘪, 𝘸𝘢𝘻𝘦𝘦 𝘱𝘢𝘮𝘰𝘫𝘢 𝘯𝘢𝘴𝘪 𝘯𝘢 𝘤𝘩𝘪𝘱𝘶𝘬𝘪𝘻𝘪 𝘸𝘢𝘬𝘪𝘸𝘢 𝘸𝘦𝘯𝘨𝘪 𝘱𝘪𝘢 𝘪𝘯𝘢𝘰𝘯𝘦𝘴𝘩𝘢 𝘯𝘢𝘮𝘯𝘢 𝘨𝘢𝘯𝘪 𝘪𝘵𝘪𝘬𝘢𝘥𝘪 𝘪𝘭𝘪𝘷𝘺𝘰𝘬𝘶𝘣𝘸𝘢 𝘯𝘢 𝘪𝘯𝘢𝘮𝘢𝘢𝘯𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘵𝘶𝘮𝘦𝘴𝘩𝘪𝘣𝘢 𝘪𝘵𝘪𝘬𝘢𝘥𝘪 𝘺𝘢 𝘊𝘩𝘢𝘮𝘢 𝘊𝘩𝘢 𝘔𝘢𝘱𝘪𝘯𝘥𝘶𝘻𝘪" Dkt. Migiro

0 Comments