Na Ally Mandai.
Emam Ashour ametozwa faini ya pauni milioni 1.5 za Misri, sawa na Shilingi milioni 82.1 za kitanzania na kusimamishwa kazi kwa wiki mbili pia ametakiwa kufanya mazoezi peke yake.
Hii ni kutokana na kushindwa kusafiri na timu hiyo asubuhi ya leo kuelekea Tanzania kwa ajili ya kushiriki mechi dhidi ya Young Africans, iliyopangwa kufanyika Jumamosi, ikiwa ni sehemu ya raundi ya nne ya hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa.
Mchezaji atafanya mazoezi peke yake katika kipindi chote cha kusimamishwa.

0 Comments