Home
About
Contact
Home
HABARI
MICHEZO
MAGAZETI
MAKALA
__DropDown 3
Home
SHULE ZA SEKONDARI DODOMA JIJI ZAPATIWA MADAWATI 2713
SHULE ZA SEKONDARI DODOMA JIJI ZAPATIWA MADAWATI 2713
Darasa Huru
December 30, 2025
▪️Ni Utekelezaji wa agizo la Mh. Rais Samia juu ya mazingira bora ya ufundishaji
▪️Mbunge Mavunde apongeza jitihada ya kutatua changamoto ya madawati
▪️Miundombinu ya madarasa na madawati mapya kuelekea Januari 2026 yakamilika
▪️Jiji la Dodoma lipo tayari kuwapokea wanafunzi 13,318 wa kidato cha Kwanza
Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde amekabidhi awamu ya kwanza ya madawati 2700 kwa ajili ya Shule za Sekondari za Jiji la Dodoma kufuatia maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kutaka kukamilika kwa miundombinu ya madarasa na upatikanaji wa madawati ya kuwapokea wanafunzi wapya wa kidato cha Kwanza Januari 2026.
Mbunge Mavunde amelipongeza Jiji la Dodoma kwa hatua za makusudi za kuhakikisha upatikanaji wa madawati ya kutosha zaidi ya 2713 ili wanafunzi wasome katika mazingira bora.
“Hii ni hatua kubwa katika kuboresha sekta ya Elimu ndani ya Jiji la Dodoma kwa kuweka mazingira bora ya kusomea ya wanafunzi wetu”Alisema Mavunde
Akizungumza katika hafla hiyo fupi,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Jabir Shekimweri amesema ni wajibu wa watu wote kuyatunza madawati hayo ili yawafae wanafunzi wengi kwa siku zijazo.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Fredrick Sagamiko amesema Jiji la Dodoma limejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wanasoma katika mazingira rafiki na kwamba hatua ya utoaji wa madawati 800 leo ni hatua ya kwanza ya kukamilisha madawati 2713 ili kuwafikia kundi kubwa la wanafunzi wa Jiji la Dodoma
Post a Comment
0 Comments
Social Plugin
ZILIZOSOMWA ZAIDI
TFF WATOA TAREHE RASMI YA TUZO ZA WACHEZAJI BORA NBC 2024-25
November 14, 2025
HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2025
January 10, 2026
KIKOSI CHA YANGA SC DHIDI YA SINGIDA BLACK STARS HIKI HAPA
January 09, 2026
NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2025
January 10, 2026
RAIS SAMIA AAGIZA VIJANA WALIOFUATA MKUMBO OKTOBA 29 WAACHIWE
November 14, 2025
TUTAZAME YOUTUBE
0 Comments