RIDHIWANI KIKWETE KIONGOZI MTULIVU

Ridhiwani Jakaya Mrisho Kikwete ni miongoni mwa wanasiasa vijana waliotokea kujijenga kwa utulivu, maadili ya kazi na uwajibikaji wa hali ya juu. Alizaliwa mwaka 1979 huko Msoga, Chalinze, Ridhiwani ni Mtoto  wa kwanza wa Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete, lakini safari yake ya uongozi haikubebwa kabisa na jina la Baba yake, Ila amejijenga mwenyewe kwa  juhudi zake binafsi, nidhamu na ushindani wa kawaida aliokuwa akikumbana nao kwenye medani za siasa.

Ridhiwani Kikwete alipitia elimu yake ya msingi na sekondari hapa Tanzania hadi kupata shahada ya masuala ya sheria na utawala. Elimu hii imempa uwezo wa kufikiri kwa kina, kutatua changamoto na kusimamia misingi ya haki na utawala bora, Sifa ambazo zimeonekana wazi katika uongozi wake.

Safari ya Ridhiwani kikwete kisiasa iliibuka rasmi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akianza na nafasi za chini kabisa katika jumuiya na matawi ya chama. Kupitia uaminifu wake na uwezo wa kufanya kazi na watu wa rika tofauti tofauti, alipanda ngazi hadi kutoa mchango mkubwa katika siasa za vijana nchini na baadae kuingia Kwenye kamati mbalimbali za CCM.

Mwaka 2015, Ridhiwani alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze baada ya mbunge wa wakati huo kufariki, Nafasi ambayo ameitumikia kwa uadilifu na ufanisi mkubwa, amekuwa karibu na wananchi, msikivu na mwenye maono mema kwa kijamii. Katika kipindi chake cha ubunge, amejikita hasa katika mambo mbalimbali kama: Kuendeleza miundombinu, Kuimarisha huduma za afya, Kuongeza upatikanaji wa maji safi na Kusaidia vijana na wanawake kiuchumi.

Ridhiwani Kikwete amejijengea taswira ya kiongozi mwenye mtulivu, Umakini na asiye na majivuno pia ni kiongozi anayetumia muda zaidi kufanya kazi kuliko kutafuta sifa. Ni miongoni mwa viongozi wachache ambao wanaendelea kupata heshima kutokana na ukaribu wao na wananchi na uwezo wa kutatua kero kwa vitendo, si kwa maneno.

Kwa sasa ameteuliwa kuwa Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora..

Hongera sana Mhe. Ridhiwani Kikwete  mwanga wako katika uongozi unaendelea kung’aa, na safari yako inatia matumaini kwa vizazi vinavyokuja, Kongole kwako kaka.

Post a Comment

0 Comments