MBETO:OMO NA JUSSA NI VIRUSI HATARI KWA AMANI ZBAR

Na Mwandishi  wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa na matamshi yanaoendelea kutamkwa na Viongozi wawili wa ACT  Wazalendo  wanaotumia Siasa za  Ubaguzi, Ukabila na Asili za watu kama Sera za chama hicho .

Imetajwa aina ya Siasa, Mahubiri na Sera hizo ni hatari kwa Ustawi wa Maisha ya Jamii na Mustakabali wa Usalama wa  Taifa. 

Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati  Maalum  ya NEC Zanzibar , Idara  ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis aliyewataja Makamu Mwenyekiti wa   ACT Ismail Jussa Ladhu na Mgombea Urais  Othman Masoud Othman  ni virusi hatari kwa  umoja Zanzibar  .

Mbeto  alisema  Jussa na OMO ni  Wanasiasa waumini wa Sera na Siasa za kibaguzi  Zanzibar  wakitumia  kama mtaji wa kisiasa wakitaka wakubalike katika jamii .

Alisema Wanasiasa hao wana ajenda  ya kuirudisha Zanzibar  katika  zama za  Ukoloni uliowaweka watu katika  makundi na mitazamo ya matabaka ya Rangi, Asili na Ukabila. 

"ACT  kimeshindwa kutaja  sera zake mbele ya Wananchi. Hivyo kimeamua kupandikiza Chuki, Ukabila na kutaja  Asili za watu. Ni Jussa na OMO wanaotaka  kuipasua jamii  "  Alieleza  Mbeto 


Katibu huyo Mwenezi aliongeza, ili nchi iwe na Utaifa lazima kuwe na Amani,Umoja na Mshikamano  ,lakini chini ya  mpango  mkakat huo,  ACT , kimekusudia  kuigawa jamii. 

" CCM kinalaani matamshi ya viongozi  hao kwa sauti ya juu. Ubaguzi, Ukabila na kutaja  Asili  za watu  ni  hatari katika jamii . Othman na Jussa wameshindwa kuwashawishi  wananchi kwa hoja na sera  " Alieleza Mbeto 

Katibu huyo Mwenezi  alisema Siasa au Sera za Ukabila,Rangi za watu  na Asili ni kwenda kinyume  na  Sheria  Namba 5 ya Mwaka 1992 ya Usajili wa Vyama vya Siasa nchini. 

Mbeto alisema  Sheria  hiyo  inapiga marufuku Vyama  kujihusisha na  Sera za  ukabila, kutumia alama  au majina ya vyama vya zamani na  aina yoyote ya Ubaguzi . 

"Tunalaani kuwasikia ACT  wakiwabagua wenzao kwa nasaba na ukabila . Kinachoendelea katika majukwaa ya kampeni  ya ACT ni  kuiyumbisha jamii na kupandikiza chuki " Alifafanua Mbeto 

Hata hivyo, CCM kimeyaita matamshi  hayo  hayana dhamira njema ingawaje wananchi wamewashtukia viongozi  wa chama hicho kutaka kuirudisha tena  Zanzibar katika misukosuko


Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form