SERIKALI YAZINDUA MWONGOZO WA KUWAINUA KIUCHUMI WAJANE

 Maelfu ya wajane kutoka Wilaya mbalimbali Mkoani Iringa wameungana katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani ikiwa lengo ni kutambua mchango wa Wajane katika jamii pamoja na kuangazia changamoto zinazowakabili.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mwongozo mpya wa uratibu wa wajane ambapo Kilele cha Maadhimisho hayo yamefanyika Mkoani Iringa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu Dkt.Dorothy Gwajima amesema serikali imeahidi kuongeza jitihada za kuwalinda na kuwawezesha kiuchumi kundi hilo la Wajane kwa kuwapa huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo za afya, ushauri wa kisheria pamoja na msaada wa chakula na mavazi kwa kushirikiana na mashirika ya kiraia.

Nae mkuu wa wilaya ya kilolo Rebeka Sanga akimuwakilisha mkuu wa Mkoa wa iringa,amesema Maadhimisho hayo yanalenga kutambua mchango wa Wajane duniani na kuwapa haki sawa pamoja na kuhamasisha jamii kutambua na kuheshimu haki za wajane hasa katika masuala ya urithi, ajira, na ustawi wa familia zao.

Nae mmoja wa wajane mkoani Iringa ameishauri jamii kuhakikisha wanaandika wosia ili kuondoa migogoro kwa familia pindi wazazi wanapofariki.

Siku ya Wajane Duniani huadhimishwa kila ifikapo Juni 23, kila mwaka ikiwa ni fursa ya kuangazia hali ya kundi hilo ambalo mara nyingi husahaulika katika mipango ya maendeleo, licha ya mchango wao mkubwa katika jamii.

Post a Comment

0 Comments