Aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini mara mbili katika
utumishi wake wa umma, akimteua kuwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na baadaye Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Akizungumza
leo Juni 24, 2025, kwenye Jukwaa la Wanawake lililofanyika katika Ukumbi
wa Kimataifa wa Mikutano (AICC) jijini Arusha, Makonda amesema hakuwa
akitarajia kuwa hiyo ingekuwa hotuba yake ya kuaga ndani ya mkoa huo.
“Balozi
(Dk Emmanuel Nchimbi), naomba kwa unyenyekevu mkubwa unifikishie salamu
kwa Rais Samia kwa kuniamini mara mbili ndani ya utumishi wake wa urais
tangu mwaka 2021, kuniteua kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi na Mkuu
wa Mkoa wa Arusha…Sikutarajia leo itakuwa hotuba yangu ya kuaga,”
amesema Makonda.
Mgeni rasmi katika jukwaa hilo alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi.
0 Comments