Mwanadiplomasia
wa Uchumi, Mtaalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), na
Mtaalam wa Hali ya Hewa, Mussa Kidato, ametangaza nia ya kuwania Ubunge
wa Jimbo la Handeni kwa lengo la kuwatumikia wananchi kwa ufanisi na
kuendeleza juhudi za maendeleo katika nyanja mbalimbali.
Kidato,
ambaye pia ni mwanasiasa mkongwe ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
anatajwa na wakazi wa Handeni kuwa ni mtu sahihi kwa wakati huu,
kutokana na rekodi yake ya kujitolea, uchapakazi, na uzoefu wa kisiasa
uliotandaa kwa zaidi ya miongo miwili.Kidato si jina geni kwa
wakazi wa Handeni. Anakumbukwa kwa ujasiri wa kuanzisha miradi ya
kijamii tangu miaka ya 90, ikiwa ni pamoja na kuwa miongoni mwa watu wa
kwanza kuanzisha huduma za usafiri wa abiria Handeni mjini, kwa mfumo wa
"safiri kwanza, lipa ukifika", pamoja na kuleta mashine ya kwanza ya
kusaga katika eneo hilo.
Kwa upande wa chama, amewahi kuwa
Kiongozi wa UVCCM Tawi (1997), Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM
(2004), Mjumbe wa TUGHE Tawi la Makao Makuu (2005), Mjumbe wa Kamati ya
Siasa Wilaya ya Handeni (2017), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya
ya Handeni (2017) na Msaidizi/Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Hali ya Hewa (2019).
Katika nafasi hizo, Kidato amekuwa kiungo
muhimu kati ya wananchi na taasisi mbalimbali, akiwasemea vijana,
akisaidia kuhamasisha miradi ya TEHAMA, mazingira na elimu ya hali ya
hewa vijijini.
Kidato amesema yupo tayari kushirikiana na
wananchi wa Handeni ili kuinua uchumi wa wananchi kupitia ushirikiano na
sekta binafsi kwa ajili ya ajira kwa vijana, Mipango ya TEHAMA kwa
elimu na kilimo, kuibua miradi ya vyanzo vya maji, barabara na afya, na
kujenga Handeni ya kisasa kupitia maendeleo ya kiuchumi yanayogusa
maisha ya kila mmoja
0 Comments