Mtume Boniface Mwamposa pamoja na Mchungaji Tony Kapola wamemtembelea na kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Viongozi hao wa dini walifika Kizimkazi leo Septemba 8, 2026, kutoa pole kufuatia kifo cha mume wa Rais Samia, Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia Septemba 7, 2026 katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar.
Katika ziara hiyo, Mwamposa na Kapola walitoa salamu za pole pamoja na faraja kwa Rais Samia na familia yake katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Ziara hiyo imekuja ikiwa ni sehemu ya mshikamano na faraja kutoka kwa viongozi wa dini kwa Rais Samia na familia yake kufuatia msiba huo.
.jpeg)
0 Comments