Yanga imemtambulisha rasmi kiungo Fred Ngoma kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa mashindano.
GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA YAKO CHUMBANI,MALIPO BAADA YA MATOKEO
Ngoma amesajiliwa kuongeza nguvu katika eneo la kiungo baada ya kusaini mkataba na Yanga
Katika utambulisho huo, Yanga pia imethibitisha kuwa Fred Ngoma atavaa jezi namba 6, namba ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa klabu hiyo.
"Leo tunamtambulisha mchezaji muhimu sana.Mnafahamu kuwa katika kipindi cha hivi karibuni tumekosa huduma sahihi ya kiungo namba sita wa kiwango tulichokuwa tunakihitaji. Tunajua tumekuwa na kiu kubwa ya kuziba pengo hilo. Tumejaribu kufanya mabadiliko kadhaa katika nafasi hiyo, lakini hatukufanikiwa kupata ubora ambao tumeuzoea na ambao mashabiki wetu wamekuwa wakiutarajia. Niwahakikishie leo kuwa mchezaji ambaye tumesamjili tuna matumaini makubwa na ufanisi wake" Injinia Hersi Said.



0 Comments