TANZANIA INAONGOZWA KWA MISINGI ILIYOASISI TAIFA – MBETO


                         Na Mwandishi  wetu,Zanzibar 

 Chama Cha Mpinduzi kimesema kama wakati   ambao  Rais Ali Hassan Mwinyi alipoachiwa uongozi na Mwalimu Julius Nyerere Mwaka 1985, hakurithi urais tu bali pia   alibeba jukumu la kujenga nchi yenye  Umoja na  uaminifu.

GUSA HAPA,UREJESHE HESHIMA CHUMBANI NA SUPER CHASI KIBOKO YA NGUVU  

Aidha ndivyo Rais Dkt  Samia Suluhu  Hassan alivyoichukua nchi toka kwa wenzake  waliomtangulia na kuifikisha katka haiba ya  maendeleo yanayoonekana  sasa.


Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar ,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo,Khamis Mbeto  Khamis,  ameeleza hayo  huku akisifu juhudi na  uongozi  wa Rais  Dk Samia  tokea aingie madarakani. 

Mbeto  alisema kama ambavyo Mwalimu Nyerere alivyoipa heshima  Tanzania duniani kote , kwa kuwa huru na utambulisho wake kisiasa kupitia siasa ya Ujamaa na kujitegemea,ndiyo kazi inayoendelezwa na Rais wa Awamu ya sita. 

Alisema kwa kufuata nyayo zile zile na kama kila kiongozi alivyoondoka   madarakani kama alivyofanya muasisi  wa Taifa la Tanzania,  na waliomfuatia baadae wote wamerithi wakipita  njia yake..

"CCM ni chama cha siasa mfano Barani  Afrika na duniani kote.Si kwa upande wowote  wa Jamhuri ya Muungano ametokeza Rais aliyetaka kuongeza muda wa kubaki madarakani akafanikiwa  "Alisema Mbeto. 

Kadhalika Katibu Mwenezi  huyo ameeleza kuwa ,wakuu wote wa nchi  baada ya Mwalimu  Nyerere ,  wameendeleza  aina ile ile ya siasa yetu  ,  diplomasia ya kiuchumi na uhusiano wa Kimataifa 

"Ni fahari ilioje kwa Rais Samia kualikwa  Angola kuzindua hospitali ya Rufaa iliopewa jina la mwalimu Nyerere. Ziara hiyo imeithibitishia  dunia thamani ya mchango wa  Tanzania na kuheshimika jina la  Mwalimu Nyerere " Alieleza Mbeto 

Pia Mwenezi  huyo aliongeza kusema hivi  karibuni Rais Dk Samia akiwa nchini Urusi, aliihakikishia dunia kuwa Tanzania ni rafiki na mshirika  wa Mataifa  yote duniani isiofungamana na siasa ya upande wowote. 

"Taifa letu ni huru na uhuru wake umetumika kuwanufaisha  wengi duniani. Tumepinga ubaguzi wa aina yoyote huku  tukipigania haki  za binadamu  bila kuyumba. Tutalinda heshima hiyo na kujivunia"Alisisitiza Mwenezi  huyo.

Akizungumzia upande  wa Zanzibar, Mbeto alisema vipindi vyote  vilivyotangulia vimetimiza wajibu  na kuivusha kiuchumi  Zanzibar hadi mahali ilipofikia. 

Hata hivyo alimpa sifa  nyingi Rais wa Awamu ya Nane Zanzibar Dk Hussein  Ali Mwinyi kwa kuiendeleza Zanzibar na kuleta mageuzi makubwa ya kisiasa na Kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments