SIMBA YAPASUKA SIMBA DAY,ELVIS RUPIA AWAUMIZA DAKIKA JIONI

 Simba SC imemaliza Simba Day 2026 kwa matokeo ya kushtukiza baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Kenya Police FC katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa leo kwenye uwanja wa uhuru,Dar es Salaam.

Mchezo huo uliokuwa sehemu ya kilele cha Simba Day 2026 ulikuwa na ushindani mkubwa, huku timu zote zikionyesha kiwango kizuri na kufanya mashambulizi ya kusaka bao.

Kwa muda mrefu wa mchezo, Simba ilijaribu kutengeneza nafasi za kufunga, lakini ilishindwa kutumia fursa zilizopatikana mbele ya lango la Kenya Police.

Dakika za mwisho za mchezo ndizo zilizoleta mabadiliko makubwa kwenye scoreboard ambapo Elvis Rupia aliifungia Kenya Police bao la ushindi dakika ya 90+, na kuifanya timu hiyo kuondoka na ushindi wa 1-0.

Hadi filimbi ya mwisho, Simba SC haikuweza kupata bao la kusawazisha, hivyo Kenya Police kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa.

Matokeo ya mwisho:

🔴 Simba SC 0-1 Kenya Police FC

⚽ Elvis Rupia 90+

Matokeo hayo yanakuwa pigo kwa Simba katika sherehe za Simba Day 2026, huku mashabiki wakitarajia kuona timu yao ikipata ushindi kwenye mtoko wa leo.

Post a Comment

0 Comments