Mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga SC, Peter Shalulile, ameanza vibaya na kwa kishindo maisha yake mapya ndani ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27, baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi mnene wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa msimu.
GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA CHUMBANI NA VIKSI LOTION
Nyota huyo wa kimataifa kutoka Namibia aliyejiunga na Yanga hivi karibuni baada ya kuachana na m Mamelodi Sundowns alionyesha kiwango cha juu na kuthibitisha ubora wake kama mmoja wa washambuliaji hatari zaidi barani Afrika. Shalulile hakuwa tu msumbufu kwa mabeki wa Namungo katika kipindi chote cha mchezo, bali pia alihusika moja kwa moja katika kutengeneza nafasi kabla ya kupiga msumari wa mwisho uliogongelea ushindi wa 'Wananchi'.
Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, uliishuhudia Yanga ikitawala sehemu kubwa ya kiwanja na kupata mabao yake matatu, huku Shalulile akihitimisha karamu hiyo kwa kufunga bao la tatu lililowahakikishia Yanga pointi tatu muhimu za ufunguzi wa msimu.
Ushindi huo wa 3-1 unaweka msingi mzuri kwa Mabingwa hao Watetezi katika mbio zao za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku mwanzo huu mzuri wa Shalulile ukileta matumaini makubwa kwa mashabiki wa Yanga kuelekea mechi za ndani na zile za Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League

0 Comments