NETANYAHU AUKATAA MPANGO WA TRUMP KUHBUSU GAZA

 Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hawakubaliani na mpango wa Gaza uliotangazwa na Marekani na kuungwa mkono na kundi la Hamas na kupingana kwa kiasi fulani na mshirika wake Rais Donald Trump.

Waziri Mkuu Netanyahu ameutupilia mbali mpango huo, kuhusu Gaza uliotangazwa na Rais Trump mwezi uliopita na kusisitiza kwamba Jeshi la Israel halitaondoka wala kuondoa chochote kwenye eneo hilo la Kipalestina hadi Hamas itakaponyang'anywa kikamilifu silaha.

Netanyahu aliliambia Baraza la Mawaziri kwamba Israel imeukataa waraka huo wa vipengele 15 ingawa alisema bado wanajadiliana na Marekani mikakati kwa ajili ya Gaza, matamshi ambayo pia aliyatoa wiki iliyopita.

“Kuhusiana na masuala fulani yanayojitokeza kwenye taarifa za habari hivi karibuni, nataka kusahihisha hapa: Israel inakataa hati ya vipengele 15. Nilisikia watu wakisema: 'Haukusema.' Kwa hivyo nasema tena: Israel inakataa hati ya vipengele 15 IDF haitaondoa chochote hadi Hamas itakaponyang'anywa silaha. Na ninaposema kuwanyang'anya silaha Hamas, namaanisha silaha nzito, silaha zisizo nzito.... silaha zote," alisema Netanyahu.

Netanyahu pamoja na kuukataa mpango huo bado alimuelezea Trump kuwa ni "rafiki mkubwa zaidi wa Israel katika Ikulu ya White House," ingawa aliweka wazi kuwa alikuwa tayari kumpinga pale inapotakikana, na kuongeza kuwa Israel tayari ilikuwa imewasilisha pingamizi kwa Marekani.

Alipouwasilisha, alisema kwamba vikosi vya Israel vingeondoka baada ya zoezi la kuwapokonya silaha Hamas kukamilika. Vikosi hivyo vinadhibiti zaidi ya nusu ya eneo hilo dogo la Palestina lenye kama wakaazi milioni 2 na ambalo kwa kiasi kikubwa limeharibiwa na mashambulizi ya Israel.

Post a Comment

0 Comments