MTOTO WA MUSEVENI KUGOMBEA URAIS 2031

 Mkuu wa Jeshi la Uganda, Muhoozi Kainerugaba, ametangaza nia ya kuwania Urais wa Uganda mwaka 2031, akisema anaamini ataweza kushinda kwa asilimia 90 iwapo atapata msaada wa baba yake, Rais Yoweri Museveni.

Muhoozi, mwenye umri wa miaka 52, ni mtoto wa Museveni ambaye amekuwa Rais wa Uganda tangu mwaka 1986 ambapo amejulikana pia kwa kauli zenye utata kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo vitisho dhidi ya kiongozi wa upinzani Bobi Wine.

Katika ujumbe wake aliyo uchapisha katika ukurasa wake kwenye mtandao wa X, Muhoozi amesema “Nitawania nafasi ya juu zaidi nchini mwaka 2031, na tutashinda kwa neema ya Mwenyezi Mungu,”

Muhoozi aliwahi kutangaza nia ya kuwania Urais katika uchaguzi wa Januari 2026, lakini baadaye alijiondoa na kumuunga mkono baba yake, ambaye alichaguliwa tena licha ya upinzani na mashirika ya haki za binadamu kukosoa hatua za serikali dhidi ya wapinzani.

Post a Comment

0 Comments