Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla,amesema taarifa inayosambaa ikimtaja kuwa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Simba SC si halali, akieleza kuwa mchakato huo haukufuata Katiba ya klabu na kwamba hakushirikishwa.
GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA YAKO CHUMBANI,MALIPO BAADA YA MATOKEO
Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Agosti 2, 2026, Makalla amesema akiwa mwanachama wa Simba anatambua taratibu za Katiba ya klabu kuhusu namna ya kupatikana kwa wajumbe wa Baraza la Wadhamini, hivyo uteuzi huo ni batili.
Wakati huo huo, Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, kupitia Mwenyekiti wake Crescentius Magori, imesema kikao kilichofanyika Bunju hakikuwa Mkutano Mkuu Maalum halali wa klabu, hivyo maamuzi yote yaliyotolewa katika kikao hicho ni batili na yanakinzana na Katiba ya Simba.
Kwa mujibu wa Bodi, Katiba ya Simba ya mwaka 2018 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2026 inaelekeza kuwa Mkutano Mkuu Maalum huitishwa na Mwenyekiti wa Klabu kwa kushirikiana na Bodi ya Wakurugenzi.
Aidha, Bodi imetangaza kuwa itakutana Agosti 3, 2026 kujadili agenda ya Mkutano Mkuu Maalum wa Wanachama, huku tarehe rasmi ya mkutano huo ikitarajiwa kutangazwa baadaye.

0 Comments