NA HERI SHAABAN( CCM ILALA)
JUMUIYA ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala imekamilisha mchakato wa taratibu za upimaji eneo la ujenzi wa nyumba ya Mtumishi Kata ya Zingiziwa Mkoani Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mtiti Mbasa, amesema kupitia Kamati ndogo ya usimamizi wa mali za Jumuiya kwa kushirikiana na Wataalam wa upimaji ardhi kutoka Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam wamekamilisha taratibu za upimaji eneo la Hekari tano na kuhakiki nyumba ya Mtumishi.
"Idara ya ardhi Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kitengo cha upimaji kilifika kupima upya na kupanda mawe kuweka na BICONS kwa ajili ya kuliharalisha eneo liwepo kisheria na liweze kupatiwa hati miliki"amesema Mtiti.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mtiti Mbasa ,amesema kazi hiyo wameshirikiana viongozi wote wa Jumuiya ya Wazazi ya Kamati ya Utekelezaji ,Baraza la Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala likiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe .
Amesema upimaji huo ulifanyika Agosti 4 mwaka huu kata ya Zingiziwa Chanika Mtaa wa Gogo sasa hivi hatua iliyofuata wakabidhiwe hati miliki.
Akizungumzia Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Katibu Mtiti Mbasa amesema Jumuiya ya Wazazi ipo salama kuanzia ngazi ya matawi mpaka kata wanaendelea kuongeza wanachama na kujenga Jumuiya .

0 Comments