JARIBIO LA UBAKAJI NJOMBE KUCHUNGUZWA

 Jeshi la Polisi mkoani Njombe limesema linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio la mwanamke mwenye umri wa miaka 38, ambaye anadaiwa kujaribiwa kubakwa na mwanaume mmoja aliyekuwa amevalia mavazi ya kike.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo limefika katika vyombo vya dola na Polisi imeanza kufuatilia mazingira yote ya tukio hilo ili kubaini ukweli na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Bangahumo, amewataka wananchi wenye taarifa sahihi zinazoweza kusaidia uchunguzi wa tukio hilo kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

Kamanda Bangahumo amesema ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kuwabaini na kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pindi wanapobaini matukio yanayoweza kuhatarisha usalama wa jamii.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, na hatua zaidi za kisheria zinatarajiwa kuchukuliwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi na kubaini ukweli wa kilichotokea.

Post a Comment

0 Comments