HECHE:SIKU YA LEO NI NYEUSI,HATUTA PIGA GOTI

 Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, amesema leo Agosti 21, 2026 ni “siku nyeusi” kwa chama hicho, kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumkuta Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili.

GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA CHUMBANI NA TIBA LISHE SASA 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Heche amewataka viongozi na wanachama wa CHADEMA kuwa na moyo wa kuendelea na shughuli za kisiasa kwa ari, ikiwemo kufanya mikutano ya hadhara pamoja na vikao vya ndani vya chama.

Heche amesema licha ya uamuzi huo, CHADEMA itaendelea kuwa imara katika misimamo yake na haitabadilisha msimamo wake, akisisitiza kwa kauli kwamba, “hatutapiga magoti.”

Aidha, amewataka wanachama wa chama hicho kuendelea kuwa na umoja na kuimarisha shughuli za kisiasa huku wakisubiri hatua zinazofuata katika shauri hilo.

Post a Comment

0 Comments