Waziri Mkuu,
Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza kuongezwa kasi ya ujenzi wa viwanja vya
mazoezi vitakavyotumika katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika
(AFCON) 2027, ili vikamilike kwa wakati na kukidhi viwango vinavyotakiwa
na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
.jpeg)
Amesema kazi hiyo
inapaswa kufanyika kwa kasi, ikiwemo kuongeza muda wa kufanya kazi pale
inapobidi, ili viwanja vikamilike kwa wakati na Tanzania iwe tayari
kabla ya ukaguzi wa maandalizi unaotarajiwa kufanywa na CAF.
Waziri
Mkuu ametoa maelekezo hayo leo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
viwanja vya mazoezi vya Farasi na Leaders Club jijini Dar es Salaam,
ambavyo ni miongoni mwa viwanja vitakavyotumika katika maandalizi ya
mashindano ya AFCON 2027 yatakayofanyika kwa ushirikiano wa Tanzania,
Kenya na Uganda.
Amesema Tanzania haipaswi kusubiri hadi dakika
za mwisho kukamilisha maandalizi yake kwa sababu CAF inahitaji
kujiridhisha mapema kuwa miundombinu inayohitajika iko tayari.
Dkt.
Mwigulu amesema mashindano ya AFCON hayapaswi kutazamwa kama tukio la
michezo pekee, bali ni fursa kubwa ya kiuchumi ambayo Tanzania inapaswa
kujiandaa kuitumia kikamilifu.
Katika ukaguzi huo, Waziri Mkuu
pia ametoa maelekezo ya kushughulikia malalamiko ya wafanyakazi
wanaoshiriki ujenzi wa viwanja hivyo, hususan kuhusu mikataba ya ajira,
malipo ya muda wa ziada na stahiki nyingine.
0 Comments