Mkazi wa Ndembezi, Manispaa ya Shinyanga,Mzee Boaz Daud Tungu (97), ambaye inadaiwa alijenga kaburi lake mwenyewe mwaka 2017, amefariki dunia na kuzikwa katika kaburi hilo kama alivyoelekeza kabla ya kifo chake.
GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA YAKO CHUMBANI,MALIPO BAADA YA MATOKEO
Akizungumza wakati wa mazishi yaliyofanyika leo Agosti 2, 2026, mmoja wa watoto wa marehemu, Robert Boaz, amesema baba yao aliamua kujenga kaburi hilo na kuielekeza familia kuwa siku atakapofariki dunia azikwe humo.
Robert amesema mwaka 2017 familia ilikusanyika nyumbani kusherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, lakini baada ya kila mmoja kurejea alikokuwa akiishi, walipokea taarifa kuwa baba yao alikuwa tayari amejijengea kaburi.
Amesema baada ya kifo cha baba yao, familia ilifanya maboresho madogo kwenye kaburi hilo kutokana na kupita kwa muda, kabla ya kutekeleza wosia wake kwa kumzika hapo.
Mzee Tungu alizaliwa Aprili 13, 1929 katika Kijiji cha Nyandekwa, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, na ameacha watoto 24, wajukuu 122, vitukuu 139 na vilembwe watano

0 Comments