Jeshi la
PolIsi mkoani Mwanza linamshikilia Mdamo Masalu Nyalwisila (40) dereva
wa gari lenye namba za usajili T 885 ENK, aina ya Scania, mali ya
kampuni ya Seedco Tanzania Limited, lililokuwa likitokea Mwanza mjini
kuelekea Bariadi kwa kumgonga mtembea kwa miguu aliyekuwa anavuka
barabara kutoka upande wa kulia mwa barabara kwenda upande wa kushoto
mwa barabara, aitwaye Prosper Yusuph Msafiri, mwenye umri wa miaka 07,
mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Wita na mkazi wa
Kisesa,na kumsababishia kifo.
.jpg)
Baada ya ajali hiyo iliyotokea
katika kata ya Kisesa, tarafa ya Sanjo, wilaya ya Magu, katika Barabara
Kuu ya Mwanza-Musoma, wananchi waliokuwepo eneo hilo walifunga barabara
hiyo na kuzuia shughuli za usafirishaji zisiendelee jambo
lililosababisha adha kubwa eneo hilo.
licha ya viongozi
mbalimbali wa Serikali kuwaomba wananchi wa eneo hilo kuwa watulivu
wakati hatua za kisheria zitachukuliwa kwa dereva pamoja na kutekeleza
ombi lao kuweka matuta ya barabarani eneo hilo, bado wananchi walikaidi
na kuanza kurusha mawe jambo lililopelekea jeshi la polisi kulazimika
kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliokuwa wanarusha mawe na
kufanya vurugu eneo hilo kwa ajili ya kurejesha amani eneo hilo.
Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kuchukua tahadhari katika maeneo yenye makazi ya watu.
0 Comments