YANGA YAANZA KAZI YAMTAMBULISHA PACHA YAKE OKELLO

Na Ally Mandai 

Klabu ya Young Africans (Yanga) imemtambulisha rasmi mshambuliaji chipukizi Juma Issa Abushuri, maarufu kama Chuga Boy, kuwa mchezaji wake mpya akitokea Fountain Gate FC kwa mkataba wa miaka mitatu. 

Chuga Boy anakuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa na Yanga katika dirisha kubwa la usajili la msimu wa 2026/2027, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya kikosi yanayolenga kuongeza ushindani wa timu hiyo katika mashindano ya ndani na kimataifa msimu ujao. 

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 amejizolea sifa nyingi kutokana na kiwango bora alichokionyesha akiwa na Fountain Gate FC katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo aliwavutia wadau wengi wa soka kwa kasi, uwezo wa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi za mabao. 

Usajili wa Chuga Boy unaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa Yanga wa kuwekeza kwa wachezaji vijana wenye vipaji, huku mashabiki wakitarajia kuona mchango wake katika kuimarisha safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao kuelekea msimu mpya wa mashindano. 


Post a Comment

0 Comments