UKAME WA MIAKA 5 UMEISHA,SIMBA YATWAA KOMBE LA FA

Na Ally Mandai  

Klabu ya Simba SC imekamilisha msimu wa 2025/26 kwa kubeba kombe la pili baada ya kuichapa Azam FC goli 1-0 katika Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank.

BOFYA HAPA:UREJESHE HESHIMA CHUMBANI NA VIKSI LOTION 

Mchezo huo wa fainali ulipigwa Julai 4, 2026 katika Uwanja wa Gombani, Pemba.

Hili ni kombe la pili kwa Simba msimu huu,baada ya ya kutwaa kombe la Muungano walilolichukua Aprili 2026 baada ya kuichakaza Yanga SC goli 1-0 kisiwani Zanzibar.

Hata hivyo, Simba inamaliza msimu huu ikiwa imelikosa taji la Ligi Kuu Bara ambalo limetwaa na Yanga SC.

Baada ya ushindi huo, simbasctanzania kupitia ukurasa wake wa Instagram imeandika “Tumewapasua AzaUTO”.

Aidha, Meneja Uhusiano wa Simba,AhmeD Ally_ amesema kikosi kinarejea Dar es Salaam Julai 5, 2026. Ameongeza kuwa moja ya njia watakayopita kutoka Uwanja wa Ndege kuelekea Msimbazi ni Mtaa wa Jangwani. 


 

Post a Comment

0 Comments