MKOPO WA ASILIMIA 10 WAINUA UCHUMI WA WANAWAKE KAKONKO

 Na mwandishi wetu,Kakonko-kigoma.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, ametembelea na kukagua shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Kikundi cha Wanawake Ubihumwe, Kata ya Gwarama, Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, ambapo alipata fursa ya kujionea shughuli za uzalishaji na maendeleo ya kiuchumi zinazofanywa na wanawake wa kikundi hicho.

Kikundi hicho kilinufaika na mkopo wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa awamu tatu wenye jumla ya Shilingi milioni 22.819 (Tsh milioni 3 mwaka 2018/2019, Tsh milioni 14.819 mwaka 2021/2022 na Tsh milioni 5 mwaka 2025/2026). Mradi huo umewezesha wanawake kujiongezea kipato kupitia shughuli za kilimo, ununuzi wa mifugo na biashara ndogondogo huku ukichangia kuboresha ustawi wa familia zao.


 

Post a Comment

0 Comments