AHMED ALLY ATAMBA PAREDI YA SIMBA ITAKAA KWA SAA TATU JANGWANI

 Na Ally Mandai

Afisa Habari wa klabu ya Simba Sports Club, Ahmed Ally, ametangaza rasmi ratiba ya parade ya kusherehekea ubingwa wa CRDB Federation Cup, kufuatia ushindi wa timu hiyo dhidi ya Azam FC katika mchezo wa fainali.

BOFYA HAPA:UREJESHE HESHIMA CHUMBANI NA VIKSI LOTION  

Akizungumza katika mahojiano na Azam TV mara baada ya mchezo huo kumalizika, Ahmed Ally alisema parade hiyo itaanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Terminal 2, kabla ya kupita katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

"Paredi yetu ya kesho itaanzia terminal 2 pale Airport halafu tutapita pale Karume, tunaingia taratibu mitaa ya Kigogo Sambusa,tunapita hadi pale Jangwani ambapo tutafanya shughuli zetu kama masaa matatu hivi na baadae tutaenda kumalizia Coco Beach."

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, msafara wa Simba utapita katika maeneo ya Karume, Kigogo Sambusa na Jangwani, ambapo utasimama kwa zaidi ya saa tatu kwa shughuli mbalimbali za kusherehekea ubingwa huo kabla ya kuhitimishwa katika eneo la Coco Beach.



 

Post a Comment

0 Comments